Shirika la habari la ABNa linaripoti kuwa: Licha ya serikali ya Syria kupinga uingizwaji wa majeshi ya kigeni nchini mwake, Vifaru vyengine kumi vya Uturuki Alhamisi ya leo tarehe 25 mwezi wa 8 mwaka 2016 vimevuka mpaka kinyume na sharia kuingia Syria siku moja baada ya magaidi wa Syria wanaoungwa mkono na Uturuki kuwatimuwa magaidi wa Daesh waliojitenga na Urutuki katika mji wa Jarabulus.
Vifaru hivyo vinatarajiwa kuungana na vile ambavyo vilivuka mpaka hapo jana katika Operesheni Ngao ya Euphrates ambayo Uturuki inasema inakusudia kuwatokemeza wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh au Dola la Kiislam na wale wa Kikurdi.
Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema hapo jana kwamba mashambulio yao yamelitimuwa kundi la kigaidi la Daesh ambalo lilikuwa linadhaminiwa na Uturuki kutoka kwenye mji wa Jarabulus na magaidi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki wameripoti kwamba wapiganaji hao wa Daesh wamerudi nyuma kuelekea kusini mwa mji wa Al- Bab.
Mlolongo mpya wa vifaru ulikuwa ukirindima kwenye barabara chafu maghaibi mwa mji wa mpakani wa Uturuki wa Karkamis na kutimua vumbi hewani kabla ya kuvuka mpaka.Vifaru hivyo baadae vilifuatiwa na magari ya deraya.
Operesheni yapekee ya Uturuki dhidi ya marafiki zake wa Daesh
Operesheni hiyo kubwa kabisa kuwahi kuanzishwa na Uturuki katika kipindi cha miaka mitano na nusu ya mzozo wa Syria imeviweka nchi kavu vikosi maalum vya Uturuki na ndege zake za kivita zikishambulia maeneo ya kundi la la kigaidi la Daesh ambalo lilikuwa na uhusiano wa karibu na Uturuki na Marekani.
Ndege hizo zinasaidia mashambulizi ya ardhini yanayofanywa na mamia ya magaidi wa Syria wanaoungwa mkono na Marekani ambao hapo jana waliingia katika mji wa Jarabulus na vijiji vya jirani bila ya kukabiliwa na upinzani mkubwa.
Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildrim amekiambia kituo cha televisheni cha Haberturk katika mahojiano kwamba wapiganaji wa kigaidi wanauunga mkono na Uturuki wa Syria wamebakia katika mji wa Jarabulus na wameanza kudhibiti miji na vijiji.
Wakurdi wawe sehemu ya ufumbuzi
Hapo jana mwanasiasa mwandamizi wa Kikurdi nchini Iraq ambaye ni mjumbe wa baraza la uongozi Ali Hussein amesema vyama vya kisiasa nchini Syria havina budi kuchukuwa hatua ambazo hazitokuwa tishio kwa usalama wa kanda hiyo baada ya Uturuki kutuma vifaru vyake nchini humo.
Hussein amesema "Tumewashauri na kuwashajiisha Wakurdi walioko nchini Syria wasikubali kukiachilia hata chama kimoja au kundi moja kuhodhi na kutumia kwa hila mamlaka ya kujiamulia mambo yao. Wakurdi na Wasyria wengine wote wanaweza kushirikiana kwa faida yao ya pamoja.Inabidi wajaribu kufikia makubaliano ya kisiasa.Hawapaswi kuwa sehemu ya tatizo nchini Syria bali wawe sehemu ya ufumbuzi nchini humo."
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amemwambia waziri mwenzake wa Uturuki kwamba vikosi vya Kikurdi nchini Uturuki vimeanza kujiondoa mashariki mwa mto Euphrates ambalo ni dali kuu la serikali ya nchi hiyo baada ya kutuma vikosi vyake maalum na vifaru kuwasaidia magaidi wake kuwatimuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh.
Serikali ya Uturuki imesema hapo jana kwamba itaendeleza operesheni zake hataka kama Syria haipendi hadi hapo itakapokuwa imeamini kwamba vitisho dhidi ya usalama wake wa taifa vimedhibitiwa.
Mwisho wa habari/ 291